top of page

Usambazaji wa Lugha Nairobi
(Language Distribution in Nairobi)

Lugha Tatu Kuu za kila Kaunti Ndogo
(Three Major Languages in Each Subcounty)

(Other African Languages)

Kenyan Languages

Lugha za Nairobi: Muktadha 
(Nairobi Languages in Context)

a7ce1a0b3b705d667c1ddcdb2122c142.jpg
mapindian_edited.jpg

Lugha za Kigeni: Kongwe

Lugha za Kiarabu, Kihindi, Kiajemi, Kigujarati, Kiingereza, na nyinginezo zina historia ndefu jijini Nairobi

Languages-of-Kenya-Source-wwwethnologuecom_edited.jpg

Lugha za Kikenya

Kwa mujibu wa Sensa ya Kenya 2019 lugha na lahaja nyingi za Kikenya zinasemwa katika sehemu mbalimbali za mitaa na vitongoji

nairobi-skyline-uhuru-park-nairobi-kenya-5058754.jpg

Lugha za Kigeni: Mpya

Lugha ambazo zimenata makini ya Wanairobi hivi karibuni ni pamoja na Kichina, Kihispania

Afrika Kusini CF.jpg

Tarakwimu za Sensa 2019 pamoja na utafiti wetu zinaonyesha raia wengi wa mataifa ya kanda za mashariki, kati, na kusini mwa Afrika wamehamia Nairobi. Lugha zao zinasikika katika sehemu anuwai za Nairobi. 

africa-more-languages-than-any-other-continent_edited_edited.jpg

Mtagusano wa Lugha

Kabla ya ujenzi wa jiji la Nairobi, eneo hili lilishuhudia maingiliano ya lugha kutoka  kwa wasafiri, wafanyabiashara, wawindaji, wamisheni, na wengi kutoka maeneo tofauti dunia: Afrika, Ulaya, Esia, n.k. Lugha zao ziliingiliana na kuathiriana na za wenyeji.

Namba za Nairobi

(Nairobi by the Numbers: 17, 47, 70, 124)

Jiografia ya Lugha ya Nairobi
(The Geography of Language in Nairobi)

Nairobi ni jiji kuu na makao makuu ya serikali ya Kenya na mashirika mengi ya kimataifa. Jiji la Nairobi linapatikana eneo la kati nchini Kenya baina ya pwani ya Bahari ya Hindi na ukingo wa Ziwa Nyanza. Kaunti ya Nairobi imepakana na kaunti za Kiambu, Machakos, na Kajiado. Kaunti hizi jirani zina asilimia kubwa ya wasemaji lugha za Kikuyu, Kikamba, na Kimaa, mtawalia. Nairobi ina utajiri mkubwa sana wa lugha anuwai kutoka pembe zote za Kenya, Afrika, na dunia.
Baada ya Kenya kujinyakulia uhuru wananchi waliohamia jiji kutoka mashinani wamekuwa wakichagua kuishi mitaa fulani kutoka na sababu anuai kama vile upatikanaji kazi, gharama ya maisha, elimu, aila na lugha za wakazi wa mtaa huo, na kadhalika. Ramani hii inaonyesha lugha tatu kuu zinazosemwa na wakazi wa kila kaunti ndogo ya Nairobi. Utafiti unaendelea na tutabainisha vyema zaidi mgawanyo huu wa lugha.

Baadhi ya Maeneo Tulikokusanya Data
Select Language Sites

 Kasarani, Njiru, Westlands, Parklands, Embakasi

Lugha za Waafrika Waliohamia Nairobi
(Languages spoken by African immigrants.)

Awamu ya kwanza ya mradi huu inashughulikia wasemaji lugha waliotoka nchi lengwa za Barani Afrika. Haya ni makundi ya wanalugha ambayo hayajaangaziwa kiutafiti na mradi unakusudia kuchangia mkabala unaochanganya isimujamii na taaluma nyinginezo.

Kutokana na ramani hii ni dhahiri kwamba kuna wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaoishi pamoja na Wakenya jijini Nairobi. Jumuiya za wasemaji lugha kutoka nchi jirani za Kenya (Uganda, Tanzania, Somalia, Sudan Kusini, na Ethiopia) ni 74% ya idadi ya Waafrika waliohamia Nairobi. Aidha, jumuiya za watu kutoka DR Kongo, Kongo, Burundi na Rwanda ni asilimia 22%; Nigeria na Eritrea ni 1.4%, huku wale kutoka kusini mwa Afrika (Afrika Kusini, Zambia, na Zimbabwe) ni 1.6%.

Bonyeza nchi zilizoangaziwa kwenye ramani ili usome taarifa zaidi. (Ryan Sears, Audrey Nickels, na Profesa Mutonya walishirikiana kuiunda ramani hii darasani). Ramani ya lugha za wahamiaji imeundwa na Tyfani Fennell.

Top 3 African immigrant by subcounty_edited_edited.jpg

Lugha Kutoka Kwingineko Afrika

Lugha kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika zinasikika katika maeneo mengi ya kaunti ya Nairobi. Lugha 3 kuu kutoka kwingineko Afrika na zinazosemwa katika kaunti ndogo tofauti za Nairobi zimeorodheshwa katika jedwali hili. Asilimia zilizomo zinaashiria idadi ya wanajumuiya hao ikilinganishwa na jumla ya Waafrika wahamaji wote katika kaunti ndogo hiyo. Kwa mfano, katika kaunti ndogo ya Kamukunji lugha za Kisomali ni asilimia 56, za kutoka Uhabeshi ni asilimia 14, nazo za Uganda ni asimilia 13 ya lugha zote za Waafrika wahamaji wanaoishi Kamukunji. Uchambuzi zaidi unapatikana katika sehemu ya 'Ramani za Nairobi' ya tovuti hii.

Idadi kubwa ya wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika inaashiria hadhi ya Nairobi barani Afrika. Lugha za wahamaji hao Waafrika zinapoingiliana na lugha za Kikenya mitaani, sokoni, michezoni, shuleni, na katika shamrashamra nyinginezo, zinaathiriana na kubadilishana. Mtagusano huu wa lugha hauna budi kuongeza hulka ya kiisimu ya Nairobi na kuchangia mabadiliko ya lugha za Kiswahili, Sheng, na lugha nyinginezo. 

Wakuu wa Mradi: Mutonya na Iribe

Screen Shot 2023-07-24 at 1.36_edited.jp

Kuhusu Mradi Huu
(About this Project)

Mradi huu uliasisiwa mwaka 2020 chini ya ufadhili wa Carnegie African Diaspora Fellowship Program (CADFP). Tuzo ya CADFP ilimwezesha Profesa Mungai Mutonya wa Chuo Kikuu cha Washington University Mjini St. Louis na mwana-CADFP mwenzake, Profesa Iribe Mwangi, aliye Mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN), kubuni mikakati mwafaka ya kiutafiti inayoendeleza mradi hadi sasa. Tuzo ya CADFP 2022 iliongezea ushirikiano wa kiutafiti na kuwezesha mradi kupiga hatua muhimu.
        Lengo kuu la mradi huu ni kusawiri kwa njia ya ramani, mtagusano changamana wa lugha unaotokana na uhamiaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Aidha, mradi unaangazia hali changamana ya lugha jijini Nairobi na uhalisi wa kimawasiliano katika jiji hili kuu la Afrika Mashariki.
Tovuti hii inalenga jumuiya zifuatazo:

  • Wenyeji wa Nairobi wanaopenda kuyafahamu mazingira yao

  • Wenyeji waliohamia Nairobi kutoka nchi mbalimbali na waliokubali kuhojiwa

  • Wenyeji wa Nairobi walio na ukarimu wa kuwakaribisha na kuishi kwa amani na wenyeji wapya walio na lugha na asili tofauti.-

  • Wenyeji kutoka sehemu mbalimbali za Kenya, Afrika, waliohamia Nairobi  kusoma na kujitafutia riziki.

Mradi huu unatambua mchango wasomi, watafiti, walimu, wanafunzi, waandishi habari, na wote wanaoangazia masiala ya matumizi ya lugha jijini Nairobi. 
 

loader,gif

Washirika Wakuu

Mradi huu haungewezekana pasingekuwepo na hisani ya watu wengi na mashirika yaliyotajwa hapa chini. Watafiti wasaidizi, wahojiwa, wanafunzi wetu na wasomi wenzetu idarani, na, hususan, Mtiva Ephrahim Wahome. Sifa za mradi huu zihusishwe nao; dosari zozote ni zetu wasimamizi wa mradi.

download.png
iie-logo.png
UoN Logo.jpg
logo-KNBS.png
download.jpg
afas fingerprint logo.png
WASHU Logo.png
bottom of page