Lugha za Nairobi
Kiswahili Mjini St. Louis
Historia ya St. Louis
1050-1150CE
-
Mji wa Waamerika Asilia zaidi ya 10-20,000 kwenye mji ujulikanao sasa kama Cahokia.
-
Lugha za watu asilia
1764: Wafaransa wahamia St. Louis
1803: Amerika yanunua St. Louis kutoka wafaransa
1890: Mji mkubwa wa nne katika Amerika
1904
-
Yaandaa Maonyesho Mkuu ya Dunia (World's Fair) na Olimpiki ya Tatu (III Olympiad)
-
Waafrika kutoka Kongo na Afrika Kusini waletwa kuonyeshwa katika maonyesho ya dunia.
-
Wazulu wawili ni Waafrika wa kwanza kushiriki mbio za Olimpiki.
1940 - Mji una wenyeji zaidi ya 800,000.
1965 - Ujenzi waanza wa mnara unaoitwa Gateway Arch.
2014 - Mjini Ferguson Michael Brown auwawa na polisi. Maandamano ya kimataifa yazua vuguvugu la Black Lives Matter.
Historia ya Wanafunzi Wakenya Katika St. Louis
1961
-
Daktari Mkenya wa shirika la MEDICO (Dkt. Njoroge Mungai) alipanga ili wanafunzi watatu kutoka mjini Nairobi, nchini Kenya (James Muniu, Sebastine Wahome, Priscilla Wainana) kusomea St. Louis
-
Walipata visa ya mwanafunzi kwa miaka minne, walitumaini kukaa kwa muda mrefu zaidi ili kuendelea na masomo.
-
Walihudhuria programu ya miaka minne katika shule ya Hadley Technical
-
Walitumaini kurudi Afrika “kuwasaidia watu wao”.
-
-
Ufadhili
-
Wazazi wa Hadley waliwanunulia nauli ya usafiri kutoka Kenya
-
Halmashauri ya Elimu ya St. Louis iligharamia karo ya shule
-
Wanafunzi wawili waliishi na mwanajumuiya
-
1962
-
Wanafunzi Watatu Wakenya walifanya mazaungumzo na wanafunzi wanawake wa Chuo cha Maryville.
-
Walijadili kuhusu hamu ya Wakenya kupata uhuru.
-
Walisisitiza haja ya wataalamu – madaktari, wanasheria, na wanasayansi, harakati za uhuru.
-
Alitaja kuhusu kutoungwa mkono na Peace Corps.
-
-
Wanafunzi walipanga kusoma kwa miaka. minane katika Amerika kabla ya kurudi Kenya
1963: Muniu walikuwa mwanafunzi msaidizi chama cha Maktaba cha shule ya Hadley Technical. Alisaidia kuandaa programu (check primary source – auditorium propgram?). Programu hii ilimshirikisha Bw. William B. Pollard as a guest speaker.
1964
-
Aprili
-
Ingawa alikuwa kijana, Muniu aliwafundisha watu wazima Kiswahili katika Shule ya jioni ya Watu Wazima ya University City.
-
Alimfundisha mwalimu wake wa sayansi, aliyeitwa George Falgier.
-
-
Juni
-
Muniu alihitimu kutoka Shule ya Sekondari ya Vashon, pamoja na wanafunzi wengine 213.
-
Naibu wa Mwalimu mkuu Ralph Wardlow alimtunza Muniu tuzo la ufanisi mkuu.
-
Historia ya Wanafunzi Wakenya Katika St. Louis (Continued)
1968
-
Agosti
-
Muniu alikihudhuria chuo kikuu cha Washington (special medicine program?)
-
Muniu alikuwa msemaji katika mikutano ya Shirika la Amerika la Wanawake wa Vyuo Vikuu (AAUW).
-
Aliwashilisha kuhusu Peace Corps na UM katika Afrika Mashariki pamoja na maonyesho ya sanaa ya Kenya.
-
-
Septemba
-
Priscilla Wainana (mwanafunzi mwenza wa Muniu kutoka Kenya) aliolewa na Peter K. Karimi.
-
Walipanga kurudi Kenya baada ya Karimi kumaliza masomo katika Chuo Kikuu cha Wisconsin.
-
Muniu alishiriki harusi ya Wainana.
-
1969: Muniu alikuwa mwanafunzi wa shahada katika WUSTL. Alifundisha darasa la Kiswahili la wiki kumi na nne. Alifundisha wanafunzi waliosoma Kiswahili kwa mara ya kwanza na wanafunzi walioendelea.