top of page

Historia ya Nairobi

  • Nairobi ni jiji kuu la nchi ya Kenya.

Enkare Nyrobi

  • Jina asili la Nairobi ni Enkare Nyrobi (yaani eneo lenye maji baridi). Ni jina linalotoka lugha ya wenyeji asili wa eneo hilo: Wamasai.

  • Mwaka 1899 kampuni ya kikoloni iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa reli kutoka Mombasa hadi Kampala ilihamisha makao yake makuu kutoka Masaku hadi eneo lililojulikana kama Enkare Nyrobi.

  • Kabla mwaka 1899 eneo lijulikanalo sasa kama jiji la Nairobi lilikuwa eneo lenye masoko na kambi ya kuwafariji wanamisafara. Misafara ilikuwa na malengo tofauti na iliwajumuisha wanabiashara, wawindaji, wamisheni, na wazungu waliotumwa na nchi za Ulaya kupata habari za Afrika. Misafara iliyoanza Mombasa ilipiga guu kwa majuma na miezi kabla ya kufikia sehemu hii ya katikati mwa nchi ya Kenya.

  • ​Kama ramani iliyoko hapo chini ya takriban mwaka 1898 inavyodhihirisha kati ya nchi za Wamasai na Wakikuyu na maeneo sambamba na mito ya Gitathuru, Mathare, na Nairobi yaliwapatia wasafiri waliotumia barabara ya Sclater huduma muhimu kama malazi na chakula. Soko la Dagoretti lilikuwa miongoni mwa masoko muhimu kwa wanamisafara. 

Mji Mpya

  • Reli ilipofika Nairobi mwaka 1899, wakazi wapya na wa kwanza wakawa ni wafanyakazi na maofisa wa reli. Kama picha hii inavyoonyesha miundomsingi ilikwa sahili, ila ilikuwa kwa kasi sana.

  • Kutoka mwaka 1899 hadi 1905, taswira na hulka ya mji mkubwa wa kwanza kuibuka - ambao haukuwa wa kipwani kama vile miji ya Lamu, Malindi, na Mombasa - ilijitokeza. Mji huu wa bara ulikua kwa haraka sana kukidhi mahitaji anuai ya wakazi wapya waliokuwa na maslahi kinzani. Wahamaji kutoka sehemu za nyingi za nchi ya Kenya na kwingineko walichangia ukarabati wa miundomsingi na mahitaji anuai ya mji.

  • Ramani ya mwaka 1903 (pia kwa hisani ya McVicar 1968) inadhihirisha mambo matatu muhimu. Kwanza, reli ilikuwa kichocheo kikuu cha ukuaji wa mji, hususan miaka ya uchanga wa Nairobi. Pili, shughuli za uendelezaji wa ghala la reli na kituo cha garimoshi zilichangia upanuzi wa serikali (Govt. Offices) jeshi (B.E.A Rifles), mitaa (Lower Level Railway Housing (Muthurwa) na Government Officers' Houses (Upper Hill)), na biashara (Indian Bazaar, African Market). Hata hivyo, shughuli za reli zilichangia hulka ya ubaguzi wa rangi na kiuchumi ambao bado unadhihirika katika mpangilio wa mji na mitaa ya Nairobi. Haswa, ramani inaonyesha maeneo yaliyotengewa Waafrika, Wazungu, na Wahindi. Vilevile kuna mitaa ya wafanyikazi wa viwango vya chini, kati, na juu. Tatu, ni dhahiri kuwa wakazi watangulizi wa Nairobi walisema lugha tofauti kutoka Kenya na Afrika, Esia, na Ulaya, Kiafrika. Bila shaka mji ulikuwa na hulka ya uwingilugha. Ingawa mfumo wa kikoloni uliendeleza sera zilizotenganisha makundi ya wakazi kufuatia msingi ya kirangi, kikabila, na kiuchumi hali haijabadilika sana tangu Kenya ilipojinyakulia uhuru mwaka wa 1963. Mradi huu umebaini mgawanyiko wa kiisimu, kikabila, na hata kitaifa unaendelea pindi jiji linavyokua na kuwapata wakazi wapya. 

  • Ramani zilizorejelea hapo juu za eneo la Nairobi kabla ya ujenzi wa reli (takriban mwaka 1898), na mji ulivyokuwa miaka mitano baadaye (1903). Ramani zote mbili kwa hisani ya McVicar, 1968).

 

Kaunti Ndogo za Nairobi

  • Mwaka 2010 katiba mpya ya Kenya iliigawanya nchi kuwa kaunti 47.

  • Nairobi ni kaunti namba 047.

    • Ina idadi ya wakazi 4,397,073 

    • Imegawanywa zaidi kwa kaunti ndogo 17

      • Dagoretti, Embakasi, Kamukunji, Kasarani, Kibra, Langata, Makadara, Mathare,  Ruaraka​   Roysambu  Starehe, Westlands

 

Nairobisubs.png

Lugha Zisemazwo Nairobi

nairobi-skyline-uhuru-park-nairobi-kenya-5058754.jpg

Miongoni mwa lugha kuu zinazosemwa Nairobi ni pamoja na kutoka Kenya, mataifa mengine ya Afrika, Uarabuni, Esia, Ulaya, Amerika, na kwingineko.

Lugha za Kikenya

Kikuyu, Kiluhya (Kibukusu, Kimaragoli, Kisamia, n.k.), Kidholuo, Kikamba, Kisomali, Kikisii, Kimeru, Kigiriama, Kimaasai, Kinandi, Kikipsigis, Kioromo, n.k.

Lugha za Kutoka Kwingineko Afrika

Lugha kutoka Uganda (Kiganda, Kinyanko, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Kongo, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini, Sudan Kusini, n.k.

bottom of page